Kijana wa Miaka 18 Amuingilia Kimaumbile Mtoto ma Miezi 2 Kutokana na Imani za Kishirikina

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kijana wa Miaka 18 Amuingilia Kimaumbile Mtoto ma Miezi 2 Kutokana na Imani za Kishirikina
Jeshi la Polisi  mkoani tabora linamshikilia Kadege Thabit (18), mkazi wa Utemini wilaya ya Uyui mkoani hapa  kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa mwaka mmoja na miezi miwili kutokana na imani za kishirikina

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa,  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa  mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo na kumwingilia kinyume cha maumbile.

Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba mtuhumiwa alitenda tendo hilo baada ya kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake akidai anaenda kumnunulia maandazi.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa baada ya kumnunulia maandazi mtoto huyo alimpeleka chumbani kwake akafunga mlango ndipo akatenda unyama huo.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la polisi umebaini kuwa sababu za kufanya ukatili huo ni imani za kishirikina, na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unafanyika,” amesema

Kamanda Mutafungwa amefafanua kwamba  mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa alidai kuwa alitenda kosa hilo kutokana na maelekezo ya mganga mmoja wa kienyeji kwamba ataweza kupata mali nyingi.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad