13 Jun 2018

Kwa mara ya Kwanza Kaseja Ndondo Cup


Kwa sasa ukimtaja Juma Kaseja mashabiki wa soka wanakumbuka alivyopangua mkwaju wa penati ya Okwi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba siku ambayo ‘mnyama’ alivunjiwa rekodi yake ya kutopoteza mchezo VPL baada ya kufungwa 1-0 na Kagera Sugar.

Ukiachana na ukongwe wote na heshima aliyoweka Kaseja ndani na nje ya soka la Tanzania, alikuwa hajawahi kucheza mechi za Sports Xtra Ndondo Cup lakini kwa mara ya kwanza alikaa kwenye milingoti ya magoli ya Ndondo Cup kuidakia UV TMK ilipocheza dhidi ya Stim Tosha ‘Stamala’.“Nilikuwa sijawahi kucheza mashindano ya Ndondo, hii ni mara yangu ya kwanza nacheza. Mashindano hako poa na yanasaidia vijana kuonekana na kuwajengea uzoefu kwa sababu huku wanakutana na wachezaji wengi wenye uzoefu na mbinu nyingi”-Juma Kaseja.

Kaseja aliiongoza UV TMK kushinda 3-0 dhidi ya Stim Tosha katika mchezo wake wa kwanza Ndondo Cup.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger