Mwakyembe Aipongeza Simba Kuingia Fainal SportPesa " Kwa Hili Mmethibitisha Hamkubahatisha VPL"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwakyembe Aipongeza Simba Kuingia Fainal SportPesa " Kwa Hili Mmethibitisha Hamkubahatisha VPL"
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amewapongeza Simba kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya.

Simba imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati wa mabao 5-4 dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC ikiwa ni baada ya dakika 90 kumalizka kwa sare tasa ya 0-0.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma, Mwakyembe amefunguka na kueleza Simba wamethibitisha kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom si kwa kubahatisha mpaka kufikia hatua hiyo ya kucheza fainali na Gor Mahia.

"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Simba kwa kufanikiwa kutinga fainali ya SportPesa Super Kenya, wamethibitisha kuwa walichukua ubingwa wa ligi si kwa kubahatisha kwa soka la kiwango" amesema.

Mchezo wa fainali ya mashindano hayo utachezwa kwenye Uwanja uleule wa Afraha Jumapili ya wiki hii ambapo bingwa wa michuano hiyo atacheza dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park nchini England.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad