Obama Kutua Kenya Kutembelea Kijiji Alichozaliwa Baba Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Obama Kutua Kenya Kutembelea Kijiji Alichozaliwa Baba Yake
Taarifa ya kuifahamu leo June 22, 2018 ni kutoka Ikulu ya nchini Kenya ambapo imethibitisha Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kuwasili nchini humo katikati ya mwezi ujao.

Obama atakuwepo nchini humo kwa saa 24 tu kabla ya kupanda ndege kuelekea nchini Afrika Kusini ambako atahutubia kwenye mkutano wa 16 wa kuhusu taasisi ya Nelson Mandela.

Taarifa zinadai kuwa Obama ambaye ataambatana na mwendesha kipindi maarufu Oprah Winfrey pia atafanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kuwatembelea ndugu zake kwa mara nyingine katika kijiji cha Kogelo alikozaliwa baba yake mzazi.

Tayari wananchi wa kijiji hicho wamekwisha anza maandalizi kwa ajili ya kumpokea ndugu yao huyo kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kuwasili July 16 mwaka huu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad