Meneja Ashikwa na Kigugumizi Afya ya Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


DAR ES SALAAM: SIKU chache baada ya video inayomuonesha ‘sweetheart wa Tanzania’ Wema Sepetu akiwa hospitali kusambaa mitandaoni na kuzua gumzo kubwa, meneja wake, Neema Ndepanya amepata kigugumizi kuongelea video hiyo.

Katika video hiyo inayoonekana kuchukuliwa hivi karibuni, inamuonesha Wema akiwa katika hali ya kuumwa huku pembeni mama yake, Miriam Sepetu akimsindikiza kuingia katika chumba cha hospitali ambapo nesi mmoja anaonekana kuwapokea.

Baada ya kuvuja kwa video hiyo,Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kupata ukweli juu ya afya yake lakini kama kawaida yake simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi ‘SMS’ kwa njia ya WhatsApp haukujibiwa.


Hata hivyo baada ya hatua hiyo, mapaparazi wetu walitinga nyumbani kwa mama yake, Sinza, Meeda kwa ajili ya kufuatilia ukweli wa msanii huyo lakini napo hawakufanikiwa kwani waligonga geti na hakuna aliyetoka kuwaeleza kinachoendelea nyumbani hapo.

Baada ya kutoka nyumbani kwa mama Wema, alisakwa meneja wa Wema, Neema Ndepanya ambapo alipopokea simu na kuhojiwa kuhusiana na video hiyo, alipata kigugumizi na kudai kuwa hawezi kuongelea.

“Jamani nipo mbele ya watu hapa siwezi kuongelea suala hilo nitakutafuta baadaye tuongee,” alisema meneja huyo.

Licha ya kusema hivyo, meneja huyo hakupiga simu hadi tunakwenda mtamboni. Alipopigiwa tena hakupokea.

Hivi karibuni Wema aliwahi kuripotiwa kwenda nchini India kwa matibabu baada ya mama yake kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mwanaye amekwenda kutibiwa.

Meneja huyo huyo aliwahi kunukuliwa na moja ya gazeti ndugu na hili na kudai kuwa Wema alikwenda nchini humo kwa matibabu ya tumbo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad