Mrema awataka watanzania kumuunga mkono JPM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Watanzania wametakiwa kumuunga mkono rais John Magufuli kwa juhudi anazofanya kuimarisha uchumi na kuwahudumia wanyonge wenye shida bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa. 

Mwenyekiti wa taifa wa bodi ya Parole, Agustine Mrema amesema hayo wakati wa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kupona  maradhi ya saratani kwenye parokia  la Uomboi ya kanisa katoliki  jimbo kuu  Moshi. 

Mrema amesema kuwa tangu aingie madarakani rais Magufuli  amefanya kazi kubwa ya kuwasaidia watu wenye matatizo ikiwemo yeye kwa kumpeleka India kupata matibabu na katika hali hiyo alianzisha mchango kanisani wa ujenzi wa nyumba za mapadre wa parokia ya Uomboi kama sadaka ya kumshukuru mungu. 

Akizungumza baada ya ibada hiyo paroko wa parokia ya Uomboi Padre Juvenal Kimario amemshukuru Dkt.Mrema kwa kuanzisha mchango huo ambao zitahitajika shs.28mil/= kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. 

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo iliyokwenda sanjari na uzinduzi wa uzinduzi wa serikali ya kijiji  cha Kiraracha wamewataka viongozi wengine kuiga mfano wa kumshukuru mungu hadharani baada ya kupata shida mbali mbali.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad