Thibaut Courtois Ashinda Tuzo ya kipa bora wa Dunia -World Cup 2018

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kipa wa Chelsea na Ubelgiji ameondoka nchini Russia akiwa shujaa na mfalme, licha ya timu yake kushindwa kuingia mechi ya fainali, baada ya kutawazwa kipa bora wa michuano hiyo, iliyomalizika rasmi jana.

Kipa huyo, amekuwa na kiwango bora katika michuano ambapo katika mechi ya kwanza, aliiongoza Ubelgiji kuisulubu Panama 3-0, huku wakiitungua England mara mbili (1-0, 2-0), huku akimzuia mchezaji bora wa mashindano hayo, Harry Kane.


Courtois anayewindwa na Real Madrid, aliwabwaga kipa wa Ufaransa, Hugo Lloris na Kipa wa Croatia, Danijel Subasic. Baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Courtois aliandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter:


 "Moja ya mafanikio makubwa kabisa katika maisha ya mchezaji ni kutambuliwa na kupewa tuzo, nimefarijika kushinda tuzo ya kipa bora. Ahsanteni sana."


Makipa wengine ambao waliwahi kushinda tuzo hii, ni Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, aliyeishinda mwaka 2014. Wengine ni Iker Casillas, Gianluigi Buffon, Oliver Kahn, Fabien Barthez, na Michel Preud'homme.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad