Watu 11 wa Familia Moja Wanyongwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu 11 wa Familia Moja Wanyongwa
Watu 11 wa familia moja wamepatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba iliyo katika mji mkuu wa India Delhi, huku 10 kati yao wakiwa wananing'inia katika dari la nyumba hiyo, kwa mujibu wa polisi.

Mwanamke mmoja aliye na takribani miaka 70 alipatikana kwenye sakafu ya nyumba. Wengi wa wale waliokuwa wamekufa walikuwa wamefungwa macho na mikono nayo ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni.

Familia hiyo imeishi wilaya ya Burari mjini Delhi kwa zaidi ya miaka 20 licha ya kwamba wametokea katika maeneo ya Rajathan uku familia hiyo ikiwa inamiliki maduka mawili katika ghorofa ya chini kwenye jengo la ghorofa tatu.

“Nilipokuwa naenda dukani niliona mlango ukiwa umefunguliwa na nilipoingia ndani niliona miili ya watu hao ikiwa imening’inia katika dari uku imefungwa mikono kwa nyuma” amesema Gurchan Sigh alipokuwa akiojiwa na moja ya chombo cha habari mjini Delhi.

Uku taarifa ya awali kutoka polisi inazungumzia karatasi zenye maandishi walizozipata kwenye nyumba hiyo ambazo zinaashiria kufanyika kwa matambiko yanayoonekana kuwa na uhusiano na vifo hivyo.

“bado tunasubiri matokeo ya upasuaji, na kuwahoji majirani na kuchunguza video za CCTV eneo hilo” amesema afisa mmoja wa polisi alipokuwa akizungumza na chombo cha habari uko mjini Dehli..

Sababu za mauaji hayo pamoja na wahusika bado hazijawekwa wazi na polisi mjini Delhi imesema kutoa taarifa baada ya uchunguzi kufanyika.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad