Chama cha Rais Joseph Kabila Kumtangaza Mgombe Wake wa Urais Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha Rais Joseph Kabila kumtangaza mgombeaji urais wake leo
Mgombeaji urais atakayepeperusha bendera ya chama cha Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Joseph Kabila katika uchaguzi mkuu nchini humo Desemba atatangazwa leo Jumatano kwa mujibu wa msemaji wa rais.

Wanachama wa muungano unaojulikana kama Common Front for Congo (FCC) waliitwa kwenda kasri la rais nje ya mji wa Kinshasa jana Jumanne kwa kile kilitajwa kuwa "mkutano muhimu.

Baada ya mazungumzo hayo ya mapema jana, msemaji wa Kabila Lambert Mende, aliwaambia waanidishi wa habara kuwa mngombea atajulikana mapema asubuhi. Wakati wa mkutano wa Jumanne kwenye shamba lake, Rais Kabila aliwatubia wale waliofika bila ya kutaja hatma yake ya kisiaisa.

Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 alikataa kuandoka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati mihula yake miwili ya kikatiba ilikamilika lakini bado amekataa kusema ikiwa atawania tena.

Jean-Pierre Bemba amewalisha makaratasi ya kuwania baada ya kurejea Kinshasa wiki iliyopita kufutiaa kuondolewa mashtaka na ICCHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Jean-Pierre Bemba amewalisha makaratasi ya kuwania baada ya kurejea Kinshasa wiki iliyopita kufutiaa kuondolewa mashtaka na ICC
Baadhi ya wapinzani wake wanashuku kuwa kabila atajaribu kubaki madarakani na kuwania kwa muhula wa tatu licha ya katiba kutoruhusu hilo.

Sintofahamu hiyo imechangia kuzuka misukosuko ya kisiasa na kusababisha maandamano ya kumpinga kabila ambayo yamesababisha umwagikaji wa damu.

Jean Pierre Bemba aondolewa hatia ICC
Baadhi ya watu ambao huenda wakapendekezwa na Kabila ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo; Mkuu wa watumishi wa rais, Nehemie Mwilanya Wilondja; na rais wa bunge la taifa Aubin Minaku.

Nchi ya Jamhuri wa Demokrasia ya Congo yenye karibu watu milioni 80 haijakuwa na mabadiliko amani ya madaraka tangu ipate uhuru wake mwaka 1960.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad