Jeshi la Polisi Lamshikilia Mbunge Esther Matiko Kisa Hiki Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Lamshikilia Mbunge Esther Matiko Kisa Hiki Hapa
Jeshi la polisi , wilayani Tarime mkoani Mara, linawashikilia Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko, pamoja na mwandishi wa habari, mara baada ya kuamuru wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kusitisha kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea nchini.

Mkutano ambao pia ulihudhuriwa na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, pamoja na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) mkoa wa Geita Upendo Peneza mara baada ya zuio hilo viongozi hao waliandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii huku lawama zote wakizielekeza kwa Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi linaamuru tuache mkutano wa hadhara hapa Tarime. Mkutano wa kampeni ambao upo kwenye ratiba ya Tume ya Uchaguzi. Msimamizi wa uchaguzi kaamuru mikutano yote ya kata ya Turwa isimamishwe”, ameandika Zitto.

Www.eatv.tv imemtafuta Kamanda wa Polisi Wilayani Tarime Rorya, Henrry Mwaibambe amesema kuwa wanamshikilia Mbunge huyo kwakile alichodai kuwa alikuwa akihamasisha maandamano ya wafuasi wa Chadema.

“Msimamizi wa kituo cha uchaguzi ametuandikia barua akitutaarifu kuzuia kwa mkutano wa hadhara kwa wanachama wa Chadema kwakuwa wamesimamishwa kufanya kampeni kwa muda wa siku nne baada ya kukiuka maadili ya uchaguzi”, amesema Kamanda Mwaibambe.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad