Makontena ya Makonda Kupigwa Mnada Tena Jumamosi Hii

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makontena ya Makonda Kupigwa Mnada Tena Jumamosi Hii
Mnada wa pili wa makontena 20 yenye samani zikiwamo   meza na viti, yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, utafanyika Septemba Mosi baada ya ule wa Agosti 25 kutofanikiwa kupata wanunuzi.

Makontena hayo ambayo yamekwama bandarini yanadaiwa kodi ya Sh bilioni 1.2.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa (TRA), Richard Kayombo, amesema mamlaka hiyo imeazimia kufanya mnada wa pili Jumamosi ya wiki hii.

Alisema mnada huo utaanza saa 2:00 asubuhi kwa kufuata taratibu zote za sheria kama mnada wa awali ulivyofanyika, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa ajili ya kununua samani hizo kwa kufuata taratibu na sheria za minada.

Alisema TRA haiwezi kutangaza bei ya mnada huo kabla ya kufanyika kwa sababu ni siri, lakini wateja watakaofika watakuta bei ambayo imepangwa kwa mujibu wa sheria serikali iweze kupata mapato yake.

Aliwaomba wananchi kuondoa hofu kuhusu samani hizo na kuwataka kujitokeza waweze kununua samani hizo.

Baada ya mnada wa Agosti 25 kukwama kwa wateja kushindwa kufikia bei iliyotangazwa, Makonda alijitokeza na kusema mtu atakayenunua makontena hayo aliyosema yana samani za shule za Dar es Salaam, atalaaniwa na Mungu.

Baada ya kauli hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alimjibu Makonda   akisema makontena hayo yatapigwa mnada mteja atakapopatikana na wala hatishiki na laana zozote.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad