Mfahamu Marehemu Dada wa Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aliyekuwa dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi ya leo Agosti 19, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza alikokuwa anapatiwa matibabu.

Kushoto ni Rais Magufuli na kulia ni Marehemu dada yake Monica Joseph Magufuli.

Jana Jumamosi Rais Magufuli alimtembelea dada yake kumjulia hali akiwa amelazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ICU, ambapo Rais Magufuli alisikika akiwaambia madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwamba, hali ya dada yake ni mbaya.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ametoa taarifa za msiba huo kupitia mitandao ya kijamii ambapo ameandika, “Nasikitika kuwajulisha kuwa Dada wa Rais (John Magufuli) Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo Agosti 19, 2018 katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu,”.

Monica amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad