Papa Francis alaani unyanyasaji wa kingono uliofanywa na mapadre

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amesema yuko katika upande wa wahanga wa zaidi ya mapadre 300 waliofanya unyama wa unyanyasaji  mkubwa kingono nchini Marekani wanaoshutumiwa kuwafanyia unyanyasaji zaidi ya watoto 1000. 

Unyama  huo ulifanyika  katika  kipindi cha  miongo saba, yameeleza  makao  makuu  ya kanisa  Katoliki mjini  Vatican. 

Wahanga  watambue kuwa  papa  yuko  upande wao, imesema  taarifa  ya  Vatican baada  ya  ripoti mbaya ya jopo la mahakama nchini  Marekani  kuchapishwa  siku  ya  Jumanne inayoelezea hatua za  kuficha madhila hayo zilizofanywa  na  kanisa Katoliki. 

"Kuna  maneno  mawili yanayoweza  kueleza  hisia zinazokabili uhalifu  huu  wa  kutisha, aibu  na  masikitiko. Papa anachukulia  kwa dhati  kazi  ya  jopo  la  mahakama pamoja  na  ripoti iliyotoa. Papa analaani  bila kiasi unyanyasaji kingono watoto wadogo. Unyanyasaji ulioelezwa  katika  ripoti  ni  uhalifu  na kiroho ni wa kukemewa. 

Vitendo  hivyo  ni usaliti  wa  imani  ambayo  imewapora wale waliofanyiwa utu  wao na, pia imani  yao. Kanisa  linapaswa kujifunza  somo  gumu kutoka  yale  yaliyopita, na kunahitajika kuwajibika kwa  wale  waliofanya  vitendo  hivyo  na  wale  ambao waliruhusu  unyanyasaji  huo  kutokea." 

Hayo  ni  maneno  katika  taarifa  ya   makao  makuu  ya  kanisa Katoliki  mjini  Vatican  iliyosomwa  na  msemaji  wa  kanisa  hilo Greg Burke.  "Wale ambao  wameathirika  ndio anaowapa  umuhimu wa  kwanza,  na  kanisa  linataka  kuwasilikiza ili  kuondoa maafa haya  ya  kutisha  ambayo  yanaharibu  maisha  ya  watu  wasio  na hatia,"  taarifa  ya  Vatican imesema. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad