Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Avua Nguo zote na Kubakiwa na Nguo ya Ndani Kisa Joto Kali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Avua Nguo zote na Kubakiwa na Nguo ya Ndani Kisa Joto Kali
Picha mpya zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini zinamuonyesha Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un akiwa amevua shati akibaki na nguo ya ndani , alipokuwa ametembelea kiwanda cha usindikaji samaki

Picha hizo , ambazo zilijaza kurasa mbili za kwanza za Gazeti la Serikali Rodong Sinmn, zinamuonyehsa kiongozi huyo akikagua kiwanda cha samaki

Si tu mtindo wake wa mavazi ulioeleza hadithi ya wenye nacho na wasionacho nchini Korea Kaskazini, lakini muda ambao ziara hiyo imefanyika unaonyesha namna pyongyang inavyoshughulikia changamoto ya chakula na joto kali mashariki mwa bara Asia.

Kim Jong-un akijadiliana na maafisa kuhusu usindikaji wa samaki
Bwana Kim aliwasili akiwa amevalia shati la rangi ya kijivu, kofia pana na suruali pana.


Kutokana na hali ya hewa ya joto kali iliyofikia 37.8, aliamua kulivua shati lake na kuendelea na ukaguzi wake akiwa na nguo ya ndani akiwa ameichomekea kwenye suruali yake ya kijivu.

Lakini wakati kiongozi huyo akipata akipozwa na namna hii ya nguo, maafisa wake wengine wakiwemo maafisa wa kijeshi na viongozi wa kiwanda walibaki katika sare zao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad