Spika Uganda Amlima Barua Rais Museveni Akitaka Kuwachukulia Hatua Maofisa Usalama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Spika Uganda amlima barua Rais Museveni
Spika wa Bunge Rebecca Kadaga amemwandikia barua Rais Yoweri Museveni akimtaka achukue hatua za haraka za kukamatwa na kushtakiwa maofisa usalama waliohusika kuwatesa wabunge na wanahabari siku ya kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo Manispaa ya Arua.
Vurugu kubwa ziliibuka na mtu mmoja aliuawa na makumi kujeruhiwa baada ya wanajeshi maalumu wanaomlinda rais kuwashambulia watu kwa madai walihusika kupiga jiwe na kuvunja kioo cha gari la msafara wa Rais.
Katika barua yake ya Agosti 27, Kadaga amemwambia Museveni kwamba maofisa usalama kutoka Kamandi Maalumu ya Ulinzi (SFC - kikosi cha kumlinda rais), polisi na wanajeshi ambao waliwapiga wabunge na raia ambao hawakuwa na silaha, lazima wakamatwe na washtakiwe mahakamani haraka iwezekanavyo.
“Kama hili halitafanyika, itakuwa kazi ngumu kuendesha shughuli za serikali bungeni. Bunge haliwezi kupuuza wala kusamehe vitendo vya utesaji,” Kadaga ameeleza katika barua yake.
Siku ya kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Manispaa ya Arua, Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine,na wabunge wengine wa upinzani akiwemo mshindi Kassiano Wadri, Francis Zaake (Mityana), Paul Mwiri (Jinja Mashariki), Gerald Karuhanga (Ntungamo) na Mike Mabikke (mbunge wa zamani wa Makindye Mashariki) walikamatwa na maofisa wa polisi na jeshi wakishutumiwa kurushia mawe na kuvunja kioo cha gari la msafara wa rais.
Zaake baadaye alichukuliwa na gari la jeshi akatelekezwa katika Hospitali ya Rubaga jijini Kampala, ambako bado amelazwa akipigania uhai wake huku akiwa na majeraha makubwa, na inahofiwa anaweza kupata ulemavu wa kudumu. Alikuwa mahututi kwa siku kadhaa.
Wabunge hao wote waliteswa na baadaye wakafunguliwa kesi yenye mashtaka ya uhaini. Mahakama Kuu katika wilaya ya Gulu Jumatano iliwaachia wabunge hao kwa dhamana.
Kadaga amedokeza kwamba Zaake bado ni mgonjwa sana wakati Bobi Wine ana dalili zote za kuteswa na kupigwa na mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahalifu.
“Mheshimiwa sana, nina wasiwasi kwamba hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa kuwakamata maofisa usalama wa kikosi cha SFC (Kamandi Maalumu ya Ulinzi), wanajeshi na polisi ambao walihusika katika vitendo vya vurugu dhidi ya raia wasio na silaha,” alisema Kadaga.
Alisema vitendo vya maofisa usalama vilikiuka Sheria ya Kinga na Kuzuia Mateso ya mwaka 2012 kifungu 2 (1) (a) na (b).
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad