Uongozi wa Simba Walaani Polisi Kumshambulia Mwandishi wa Habari siku ya Simba Day

Uongozi wa Simba Walaani Polisi Kumshambulia Mwandishi wa Habari siku ya Simba Day
Uongozi wa klabu ya Simba umelaani vikali tukio la Polisi kumpiga Mwandishi wa Habari za Michezo Sillas Mbise ambeya alikuwa akikusanya habari katika tamasha la Simba Day Agosti 8 Jumatano ya wiki hii.

Kupitia Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah 'Try Again' amesema tukio hilo halifuahishi kutokana na mchango wa Wanahabari kwa ujumla juu ya mchango ambao wanatoa.

Again ametoa pole zake za dhati kwa Wanahabari wote kwa ujumla juu ya Mwandishi huyo aliyepigwa na askari hao wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alipokuwa ndani ya Uwanja kuzungumza machache kabla ya pambano kuanza.

Kitendo cha Mbisse kupigwa kilisababisha Waziri Lugola kuingia na ndipo ikafikia hatua ya Mwandishi huyo kutolewa nje ya Uwanja kwa usalama zaidi.

HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Uongozi wa Simba Walaani Polisi Kumshambulia Mwandishi wa Habari siku ya Simba Day Uongozi wa Simba Walaani Polisi Kumshambulia Mwandishi wa Habari siku ya Simba Day Reviewed by Udaku Special on August 10, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.