Vijana Njooni Niwajaze Mapesa- Cheyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vijana njooni niwajaze mapesa”- Cheyo
Mwenyekiti wa UDP taifa John Cheyo amefunguka kuwa hawezi kuhama chama alichokianzisha mwenyewe na kuhamia CCM, na kuwataka vijana kujiunga na chama chake ili wajipatie pesa.

Cheyo ambaye ni maarufu kwa jina la Bwana Mapesa amefunguka hayo kupitia Weekend BreakFast leo Jumamosi Septemba mosi, ambapo amesema kuwa siasa za upinzani zikiendelea hivi kwa viongozi wa upinzani kuhama na kupandikiza chuki wapiga kura hakutakuwa na mtu wa kumtoa Rais Magufuli madarakani.

“Siwezi hama chama kwenda kuunga jitihada ntaunga nikiwa UDP siwezi hama nyumba yangu mimi ndio baba mwenye nyumba, nawakaribisha vijana na wote wenye mapenzi na siasa waje kwangu UDP niwajaze mapesa”, amesema Cheyo.

John Cheyo ni moja ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini akiwa mwanzilishi wa Chama cha United Democratic Part (UDP).

Cheyo alipata umaarufu sana nchini katika kinyanganyiro cha uchaguzi cha mwaka 2005, ambapo alisema kwa ufupi kwamba sera zake ni "kuwajaza watanzania mapesa". Hii ilikuwa ni sera inayopendwa sana na watu kwa sababu wakati huo baadhi ya watu walikua wanalia hali ngumu ya maisha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunataka kujua kama vijana walioko sasa katika chama chake wameishajazwa mapesa au bado ili wengine wajiunge.
    UsirudieKosaKupigiaKuraUpinzani.

    ReplyDelete

Top Post Ad