Wazazi wa Miss Tanzania Waibuka na Kusema Mtoto Wao Ameokoka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wazazi wa Miss Tanzania Waibuka na Kusema Mtoto Wao Ameokoka
Baada ya mashindano ya Miss Tanzania kukamilika na Queen Elizabeth Makune kuibuka mshindi wa taji hilo kwa mwaka 2018, wazazi wake wameibuka na kusema kwamba mtoto wao ameokoka na anamtumikia Mungu.

Akiongea kupitia eNewz mama wa mrembo huyo amesema kwamba mtoto wake amekuwa akipenda sana kuvaa 'crown' tangu akiwa mdogo, kwani hata wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alikuwa anapenda kununuliwa keki ambayo ina 'crown' juu.

Hata hivyo mama Queen Elizabeth ameendelea kusema kwamba "Queen ni mtoto wa kanisa hata kabla hajawa 'star', alikuwa anakaa mlangoni kanisani kwa ajili ya kupokea na hata alipokuwa anachukua mataji mbalimbali kabla la Miss Tanzania alikuwa akienda kanisani na kuomba aombewe ili kuweza kufika mbali zaidi"

Kwa upande wake, Miss Tanzania Queen Elizabeth Makune amesema anajisikia furaha kupata nafasi hiyo na kudai atahakikisha kupambana na kuipigania Tanzania zaidi ya Miss Tanzania 2016/2018 Diana alivyokuwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad