Idris Sultan Afunguka Kuhusu Picha yake ya Utupu Iliyovuja...Amtaja Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mcheshi maarufu ambaye pia ni mwigizaji nchini Tanzaia Idris Sultan amejitetea kufuatia picha ya utupu ambayo imekuwa ikisambaa mtandaoni.

Kulingana na Idris watu wa karibu naye wanamfahamu ni mtu wa aina gani na hivyo kwa heshima yake hawezi kujidhalilisha kwa njia hiyo.

Picha inayodaiwa kuwa ya mshindi huyo wa Big Brother Afrika (BBA), imekuwa ikisambaa sana mtandaoni huku mali yake akiinadisha kwa bei rahisi.

Idris sasa anadai kuwa, ana imani aliyevujisha picha hiyo ni mchumba wake wa zamani Wema Sepetu na picha hiyo ni ya miaka miwili iliyopita.

“Wanaonipenda wanajua mimi mtu wa aina gani, ndugu zangu wanajua mimi mtu wa aina gani, marafiki zangu, mchumba wangu ananifahamu vyema sana, mashabiki wangu wananijua sanaaa hadi wakati mwingine wanajua nini nitasema kabla sijasema. Kampuni zinazonidhamini zinafahamu mimi ni mtu wa aina gani. Hii ndio nguvu niliyo nayo, ni nguvu ya mapenzi,” aliandika kupitia Instagram.

Idris anadai kuwa, watu wanaovujisha picha zake mtandaoni ni wenye nia mbaya wanaojaribu kuficha uchafu wao: Sasa ficheni uchafu wenu wa sasa kwa kuweka uchafu wangu wa miaka miwili iliyopita na mwone ni vipi Allah ataendelea kunibariki na mashabiki wangu... Sijutii, ni mitihani tu. Nakusamehe na nakuombea Allah akusamehe pia. Makosa yangu yatabaki kuwa yangu #NguvuYaMapenzi

Mchekeshaji huyo amewataka wanaofanya hivyo kuachia picha zake zote chafu hata na zile wakiwa na Wema na kisha kusema hatishiki kabisa nay a kale yatabaki kuwa ya kale.

Idris na Wema waliwahi kuwa wapenzi na hata kufanikiwa kupata ujauzito wa pacha lakini kwa bahati mbaya, mimba hiyo ilitoka na mambo yao kusambaratika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad