Indonesia Yaomba Msaada wa Kimataifa Kukabiliana na Maafa ya Tetemeko la ardhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Indonesia Yaomba Msaada wa Kimataifa Kukabiliana na Maafa ya Tetemeko la ardhi
Indonesia imeomba msaada wa jumuiya za kimatafa wakati huu ikihangaika kupata chakula sambamba na vifaa vya uokoaji katika kisiwa cha Sulawesi, ambacho kimeharibiwa vibaya kwa kimbunga na tsunami mwishoni mwa juma lililopita.

Thailand na Australia ni miongoni mwa nchi ambazo tiyari zimetoa misaada yao.

Vikosi vya uokoaji vinaendelea na juhudi za kutafuta watu waliokwama katika majumba makubwa kwenye mji wa Palu huku uwezekano wa kuwakuta wakiwa hai ukiendelea kupungua.

Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6.

Waokoaji wamekuwa wakichimba kwa mikono wakiwatafuta manusura kwenye mji wa Palu.

Vikosi vya uokoaji vinajaribu kuwafikia mamia ya watu ambao inawezekana wakawa hai katika mji wa Palu ambao miundombinu yake imeharibika vibaya huku wengi wao wakitajwa kukwama katika maduka na majumba makubwa.

Sehemu kubwa ya mji wa Palu imeharibiwa vibaya huku dalili za kuwapata walionasa wakiwa hai zikianza kufifia.

Katika ziara yake kwenye mji wa Palu Rais wa Indonesia Joko Widodo, amewaambia viongozi wa eneo hilo kuwa serikali kuu itatoa mahitaji yote muhimu ili matengenezo mapya ya mji huo yaweze kufanyika.

''Hakika hii ni hali ya dharura kama ilivyo ya Lombok. Kutakua na ugumu wakati, kwa siku moja au mbili na ni kazi kubwa. Uelekeo wa Barabara hii haipo imefungwa, ata uwanja wa Ndege haufanyi kazi ipasavyo," amesema.

"Vituo vya kuzalisha umeme pia vimeharibiwa, na kati ya saba ni viwili tu ndivyo bado vinafanya kazi na wasambazaji wa mafuta wasingeweza kuyafikia maeneo kutokana na kuharibika kwa barabara. Lakini tayari tumeagiza kila kitu kama mafuta, na wasambazaji watafika siku mbili kuanzia sasa.

"Na vifaa vyote vizito vitakuja usiku wa leo, ili tuweze kuvitumia kesho pamoja na ahueni ya misaada kama vile chakula na maji safi.Baada ya kuona kila kitu kinafanya kazi kama kawaida tutaingia kwenye hatua kujenga na kuzirekebisha nyumba hizo. Na Serikali itawaaidia kama tukivyofanya Lombok."
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad