10/11/2018

Kamanda Mambosasa: Mo Dewji Bado Hajapatikana, Oparesheni Kali ya Kumtafuta Bado Inaendelea

Polisi Yasema Mo Dewji Bado Hajapatikana, Oparesheni Kali ya Kumtafuta Bado Inaendelea
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amezungumza mchana huu kuhusiana na tukio la kutekwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mo Dewji ambapo amesema hadi mchana huu taarifa rasmi ni kwamba Mo bado hajapatikana na watekaji bado hawajakamatwa.

Mambosasa amewataka wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambaa mitaani kwamba Mo kapatika akiwa Coco beach kwa kuwa ni za uongo na wala hazijatolewa na ofisi yake.

Amesema jeshi la polisi linaendelea na Opareshen kali kwa kushirikisha mikoa mitatu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana na watekaji wanatiwa Mbaroni

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger