Makonda Atoa Amri Kali Atoa Siku 5 Kufuta Picha za Ngono Kwenye Simu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Atoa Amri Kali Atoa Siku 5 Kufuta Picha za Ngono Kwenye SimuMkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa mkoa huo kufuta picha za ngono kwenye simu zao hadi kufikia Jumatatu ijayo kabla Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hawajaanza kufuatilia.



Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatano wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tangu alipowataka wakazi wa Dar kumtumia majina ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo baada ya video ya msanii Amber Rutty kusambaa mitandaoni akifanya mapenzi kinyume cha maumbile na mpenzi wake.



“Kitendo cha kumuingilia mtu kinyume cha maumbile ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya taifa letu, lakini kuna watu wanajiuza kwenye mitandao na wanaona kwao ni jambo la kawaida, hii ni aibu kubwa.



“Ninawataka wakazi wote wa Dar es Salaam wawe wamefuta picha za ngono kwenye simu zao hadi kufikia Jumatatu kabla  TCRA hawajaanza kufuatili,” amesema RC Makonda.



Aidha, Makonda amesema ameunda kamati itakayokuwa na majukumu manne, ikiwemo kushughulika na watu wote wanaocheza picha za ngono, ambapo kwa Dar es Salaam imebainika kuna nyumba 24 zinazotumika tumeshazifahamu, wanachukua madada wanawaleswesha madawa kisha wanawafanyisha, wengine wanaingia makubaliano, wanawalipa kisha kuwarekodi na kuziuza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad