Mama Mobeto Afunguka Sababu ya Mwanaye Kufunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mama Mobeto Afunguka Sababu ya Mwanaye Kufunguka
IKIWA ni siku chache baada ya mwanamitindo Hamisa Mobeto kumwagana na mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Shufaa Lutiginga ameibuka na kutoboa siri ya bintiye kutusua, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. 



Mama Mobeto aliliambia Risasi Mchanganyiko kuwa, siri kubwa ya mwanaye kuonekana mambo kumwendea vizuri baada tu ya kuachana na Diamond ni kwa sababu amekuwa msikivu kwa kila jambo analomwelekeza.

Aliendelea kusema kwamba amekuwa akimshauri na kumwelekeza Mobeto mambo mengi sana yanayohusiana na maisha na anamshukuru Mungu kwani kwa sasa amekuwa ni mtoto msikivu sana na ameona faida yake kwani amekuwa akipata kazi mbalimbali nje ya nchi.


“Namshukuru Mungu sana kwa kila jambo kwani mwanangu baada ya kuachana na ishu za mapenzi amekuwa msikivu, anasikiliza na kuzingatia kile ninachomwambia kama mama yake na ndiyo maana anafanikiwa na anazidi kutusua kila siku,” alisema mama Mobeto. Hata hivyo, aliwashauri mastaa wa kike na wasichana wote kwa jumla kuwaheshimu wazazi wao na watu wote wanaowazidi umri pale wanapowaambia au kuwaelekeza kitu wawe wasikivu ndiyo watafanikiwa katika maisha yao.



Hamisa tangu atangaze kumwagana na Diamond amekuwa akipata dili mbalimbali za kazi nje ya nchi ambapo alianzia Kenya na hivi sasa yupo nchini Marekani akifanya shoo na mkali wa dansi nchini, Christian Bella ‘Obama’. Mrembo huyo pamoja na masuala ya mitindo, hivi karibuni alijiingiza kwenye muziki wa Bongo Fleva na kuachia wimbo wake wa Madam Hero ambao unafanya vizuri kwenye gemu.

Stori: Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad