Polisi Yakanusha Kamanda Mambosasa Kuondolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Yakanusha Kamanda Mambosasa Kuondolewa
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, amekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni zinazohusu jeshi la polisi kufanya mabadiliko na kuomba wananchi kuzipuuza.

Taarifa ya msemaji hiyo imeeleza kuwa mkuu wa jeshi hilo, IGP Simon Sirro,  amewataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma na kuwataka kuacha kutumia mitandao ya kijamii na badala yake waitumie kupeana taarifa za kuleta maendeleo.

“Serikali na vyombo vyake ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa umma,” ilisema taarifa ya Mwakalukwa.

Taarifa ambazo si za kweli  zilidai Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, wamepangiwa majukumu mengine.

Ziliongeza kusema kuwa Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii,  na Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, SACP Ramadhan Mungi,  akiwa kamanda mpya wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad