Ray Awaonya Mwana Fa, Richie Baada ya Kupata Uteuzi BASATA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ray Awaonya  Mwana Fa, Richie Baada ya Kupata Uteuzi BASATA
Msanii wa filamu nchini Vincent Kigosi (Ray Kigosi) amewataka wajumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mwana FA pamoja na single Mtambalike 'Richie' ambao wameteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, kutojisahau kwa nafasi walizopewa badala yake wakasimamie maslahi ya wasanii.

Ray Kigosi ametoa kauli hiyo alipozungumza na www.eatv.tv ambayo ilitaka kupata maoni yake juu ya hatua ya kuhusishwa kwa wasanii hao kwenye nafasi mbili za wajumbe wa bodi ya BASATA ambayo mwenyekiti wake aliteuliwa na Rais Magufuli.

Ray amesema “nimefurahi kwa uteuzi huu lakini ningefurahi zaidi kama pale BASATA na Bodi ya filamu wangekaa watu ambao wanajua kila kitu kuhusu sanaa, nimshukuru sana Waziri kwa kuwateua Mwana Fa na Richie, ila niwaambie tu wasijisahau watusemee sisi na sio wajisemee wao ili tuweze kuvuka.”

“Kwa upande wa BASATA ningewashauri wafumue zile sheria ambazo hazina mashiko, wajumbe wapunguze kutufungia lakini lazima waendane na mabadiliko ya sasa ili tuweze kuandika stori tofauti na mapenzi kwa hiyo nawashauru tena wawaambie nini maana ya sanaa.” Ameongeza Ray Kigosi

Oktoba 5 mwaka huu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harisson Mwakyembe alitangaza kuwateua wajumbe wa bodi ya basata watano wakiwemo wasanii hao wawili pamoja na Dkt Saudini Mwakaje, Asha Mshana, Dkt Emmanuel Ishengoma ambao ni wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad