Tanzia: Msanii wa Bongo Movie Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tanzia: Msanii wa Bongo Movie Afariki Dunia
Aliyewahi kuwa msanii wa maigizo wa Kundi la Sanaa la Kaole, Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Oktoba 20, 2018 majira ya saa 3, asubuhi.





Akizungumza na Global Digital, mtoto wa marehemu, Abdallah Ditopile amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema baba yake aliugua ghafla usiku ndipo wakamkimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu lakini alifariki dunia akipatiwa matibabu.



“Baba alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha na kisukari, jana alizidiwa ghafla tukamkimbiza katika Hospitali ya Amana, madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu, kutokana na hali yake kutokuwa nzuri sana alilazimika kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua ‘Mashine ya Oksijeni’.



“Lakini ilipofika asubuhi hali yake ikabadilika, madaktari walitupatia rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili Tawi la Mloganzila, wakati tukijiandaa kuita ambulance, akakata roho, baba ametutoka,” amesema Abdallah.



Kwa sasa ndugu wamekusanyika nyumbani kwa kaka mkubwa wa marehemu, maeneo ya Ilala Sokoni kwa ajili ya kupanga taratibu za msiba. Baadaye wataeleza msiba utakuwa wapi, mazishi yaafanyika lini na wapi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad