Ariana Grande Ashinda Tuzo ya Mwanamke Bora Mwaka 2018

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ariana Grande ashinda Tuzo ya Mwanamke bora mwaka 2018
Jarida la Billboard limemtaja muimbaji wa Pop Ariana Grande kuwa mwanamke wa mwaka 2018( Billboard 2018 Woman of the Year) na hivyo kukabidhiwa tuzo ya heshima December 6,2018.

Ariana Grande ameweza kushikilia chart za Billboard 200 kwa kushika nafasi ya kwanza mara tatu ikiwemo na album yake ya ‘Sweetner’ ambayo ilikaa nafasi ya kwanza mwezi wa August 2018 na kushika rekodi ya kuwa msanii wa nne wa kike kuingiza nyimbo nyingi kwenye chart za Billboard Hot 100.

 Mkuu wa maudhui ya Billboard Ross Scarano amesema kuwa Ariana Grande anastahili kupata tuzo hiyo kutokana na kutoa aina ya muziki ambao jamii inanufaika nao ikiwa na kujiamini na kusimama peke yake. Ugawaji wa tuzo hizo unatarajiwa kufanyika usiku wa December 6,2018  katika sherehe za Woman In Music jijini New York.

Ariana Grande ataungana na wakali kama Selena Gomez, Madonna, Lady Gaga na Taylor Swift ambao pia waliwahi kukabidhiwa tuzo hiyo kutokana na mchango mkubwa wa muziki wanaoufanya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad