Diamond Platinumz Aililia BASATA kuhusu wimbo wa 'Mwanza Nyegezi'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamuziki nyota nchini Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya wimbo alioshirikiana na Rayvanny, 'Nyegezi' kufungiwa na BASATA kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii. 

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Diamond Platnumz  ameandika haya: 

KWA WAZEE WANGU WA BALAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)  
Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri Mnayoifanya....lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu Nchini.....Ujumbe wenu kuhusu Kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta rizki ili kuendelea kulijenga taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekujamara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi..... 

Tuki wama Wasani ambao tumesajiliwa tuna kila haki ya kuheshimu na kutii balaza letu la sanaa BASATA pindi linapotoa tamko.....kwasababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa....na kwakutambua kuwa Sanaa ni kazi ya Ubunifu, na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa ndiomaana mliteuliwa Nyinyi wazee wetu maalum kwa jili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya Mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa ilio bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa..... 

ila Kwenye UFUNGIWAJI huu nami nilikuwa nina OMBI ama PENDEKEZO kwa balaza letu pendwa la sanaa Tanzania (BASATA)....

Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na kituo cha Mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema Kama balaza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa sio kila Nyimbo ni kwajili ya watoto wadogo....Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe Kwenye Ule muda ambao serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame.... PILI:- kusema tuifute Mitandaoni pia, naomba pia Balaza letu pendwa litutazame pia na hapo.... kwasababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sizani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuziperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata Video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na Madhara zaidi kwa watoto, kuliko hichi kinyimbo chetu cha #MWANZA NYEGEZI 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad