Hii ndio video ya kwanza Tanzania kufikisha views Milioni 16 kwa wiki kwenye mtandao wa YouTube, utashangaa msanii mwenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mara nyingi tumezoea kuona wasanii wa muziki hapa Tanzania ndio wanaoongoza video zao kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube lakini mambo yamebadilika kabisa pengine huenda watu kwa sasa wanaangalia aina ya uzuri wa content pasi kuangalia jina la muhusika.



Anyway kama wewe ni mfuatiliaji wa wachekeshaji wachanga basi utakuwa umeshawahi kukutana na mtu anaitwa Steve Mweusi, yeye ndiye Mtanzania na mchekeshaji wa kwanza mwenye video iliyotazamwa zaidi Tanzania ndani ya wiki moja (siku 7) .

Video hiyo ya vichekesho, iliyowekwa Novemba 14 mpaka leo Novemba 22 imeshatazamwa mara milioni 16+ (views milioni 16+). Na hii ndio inakuwa video ya kwanza kupata mapokezi makubwa nchini Tanzania kuliko video yoyote ile iliyowahi kuwekwa kwenye mtandao huo.



Kabla ya hapo, video zilizokuwa zinaongoza kutazamwa zaidi ndani ya wiki kwenye mtandao wa YouTube ni Salome, Kidogo, Nana zote za Diamond Platnumz,  Kwangwaru ya Harmonize na Seduce Me ya Alikiba na zote hakuna video iliyofikisha views milioni 5.

Steve Mweusi akiongea na Bongo5, amesema amepata simu nyingi na maoni kibao mtandaoni watu wengi wakihoji kama ni kweli views ni za kwake au amefanya ujanja wa kununua.

Bongo5
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad