Spika wa Bunge, Job Ndugai Ataja Wabunge, Mawaziri Vinara wa Utoro Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Spika wa Bunge, Job Ndugai Ataja Wabunge, Mawaziri Vinara wa Utoro Bungeni
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amewataja wabunge na mawaziri wenye mahudhurio madogo zaidi katika vikao vya kamati za bunge na vile vya bunge.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Novemba 15, Spika Ndugai amesema orodha hiyo inatokana na mahudhurio ya wabunge na mawaziri kwenye mkutano wa 11 kuanzia Bunge la Bajeti pamoja na mkutano wa 12.

Ndugai amesema wabunge wa mwisho kabisa na mahudhurio yao kwenye mabano kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae (CCM), Salim Turki (14%), Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi (9%) na Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema (7%).

“Kwa hiyo Arusha wajue hawana mwakilishi hapa, hata leo ameingia dakika 15 na kuondoka, majina yao nitapeleka kwenye vyama vyao,” amesema Ndugai.

Kuhusu mawaziri, wa mwisho kabisa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi (38%), Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, January Makamba (37%) na wa mwisho ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (35).

“Orodha hii inahusu vikao vyote vya kamati na bunge, unakuta kamati inakaa hakuna waziri wala naibu wake, na wala hakuna taarifa,” amesema Ndugai.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad