Wanaosema Nimeachana na Iyobo Watasubiri Sana- Aunty Ezekiel

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa filamu za Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka kuhusu mahusiano yake na Mpenzi Wake ambaye ni dancer wa WCB Moses Iyobo.

Aunty Ezekiel amefunguka na kuweka wazi kuwa amekuwa akishangazwa na tetesi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa kuwa yeye ameachana na Baba watoto wake Mose Iyobo.



Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Aunt alisema afikiri katika dunia hii hata kama unapenda na mtu kwa kiasi gani hamuwezi kuishi bila kutokea ugomvi wowote kwa sababu wao sio malaika lakini wanapogombana wanayamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida lakini inavyoonekana kuna watu wanataka kuona penzi lao likisambaratika kabisa.



Nafikiri wanaosema tumeachana watasubiri sana kama kugombana hakuna wanaoishi kama malaika, kwa sababu wote ni binadamu lakini hatuna ugomvi endelevu, yule ni mzazi mwenzangu na wanaosubiri tuachane tutawaacha mbali sana”.

Tetesi za Aunty Ezekiel na Mose kuachana Zilianza mara Baada ya wawili hao kutoonekana kwenye mitandao ya kijamii pamoja na zilipamba moto zaidi Baada ya Aunty kumuacha Mose Tanzania alipoenda kusheherekea birthday yake Dubai.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad