Waziri Mkuu: Nimefarijika Na Maendeleo Ya Viwanda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu: Nimefarijika Na Maendeleo Ya Viwanda
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa viwanda kwenye mkoa wa Tanga kwa sababu vitasaidia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.

Aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Novemba 1, 2018) alipotembelea kiwanda cha saruji cha Rhino na kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, vyote vya jijini Tanga.

Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wawekezaji wa viwanda hivyo kwa kuunga mkono mkakati wa Serikali.

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda.

Akizungumzia kuhusu kiwanda cha Rhino, Waziri Mkuu alisema kiwanda hicho na vingine vya saruji nchini vitasadia kupunguza gharama ya saruji nchini na kurahisisha ujenzi.

“Serikali inaamini kwamba uwepo wa viwanda mbalimbali nchini si tu utawezesha ukuaji wa uchumi wa Taifa, pia utasaidia katika kumaliza changamoto ya ajira hususani kwa vijana.”

Akiwa katika kiwanda cha Tanga Fresh, Waziri Mkuu aliwataka wafugaji mkoani Tanga wabadili mfumo wa ufugaji na wafuge kwa kutumia njia za kisasa ili waongeze uzalishaji.

“Wafugaji lazima wakubali kubadilika watumie fursa ya uwepo wa kiwanda hiki kwa kufuga kisasa ili wapate maziwa mengi kwa sababu wana uhakika wa kuyauza kiwandani hapa”.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka wananchi walioajiriwa kiwandani hapo wafanye kazi kwa bidii, uaminifu na wawe waadilifu na wasijihusishe na vitendo vya wizi kwa kuwa havina tija.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, NOVEMBA 2, 2018.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad