AliKiba atangaza aina mpya ya muziki ataokuja nao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa Bongo Fleva AliKiba ambaye pia anamiliki lebo yenye wasanii wanne akiwemo mdogo wake Abdukiba amefunguka kuwa wako njiani kuandaa wimbo wenye mahadhi ya mduara.


Kiongozi huyo wa kundi la 'Kings Music' amesema hayo kwenye heshima ya Bongo Fleva inayoruka kila siku za Ijumaa, kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio wakati akijibu swali la mmoja wa shabiki wake, lililohoji ni lini atafanya muziki wa aina hiyo.

"Kuhusu wimbo wa mahadhi ya mduara, tuko njiani tunaandaa wimbo mtamu. Na tunajipanga kwelikweli, yaani tutatoa kitu kweli kweli kuonesha uwezo wetu wa kufanya vitu tofauti, watu wetu mjiandae tu", amesema AliKiba.

Aidha akizungumzia kuhusu kundi lao kutoa nyimbo mfululizo amesema kuwa, "Kutoa kwetu nyimbo mfululizo sisi kama Kings Music ni dalili kuwa hii game hatuwezi kuiachia kazi ni nyingi, wategemee vitu vizuri yaani mambo ni 'bampa to bampa' mwakani kila mmoja anatoa wimbo wake na video zote tayari".

Baada ya jana kutambulisha wimbo wa mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi hilo, Cheed wimbo ambao amewashirikisha Ki2ga na Alikiba ujulikanao kama 'MASOZY'. Leo Alikiba pia ametambulisha wimbo wake mpya uneokwenda kwa jina la 'KADOGO'.

EATV
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad