Maseneta Nchini Marekani Wamuita Mwanamfalme Mohammed bin Salman Mtu Hatari na Chizi Kisa Mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maseneta Nchini Marekani Wamuita Mwanamfalme  Mohammed bin Salman  Mtu Hatari na Chizi Kisa Mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi
Maseneta nchini Marekani wanaamini pasi na shaka sasa kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman amehusika katika mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Msimamo huo wa maseneta unakuja baada ya kufanya kikao cha siri na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Bi Gina Haspel.

Seneta wa mwenye ushawishi mkubwa kutoka chama cha Republican Lindsey Graham amesema ana "imani ya hali ya juu" kuwa Mohammed bin Salman (MBS) alipanga njama ya kumuua Khashoggi.

Apandikizwa uso mpya baada ya kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi
Michelle Obama aelezea hofu amekuwa nayo kwa muda mrefu
Seneta huyo wa jimbo la Carolina Kusini amesema bin Salman ni "chizi" na "mtu hatari".

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Mkurugenzi wa CIA bi Haspel alikutana jana Jumanne na wajumbe wa Seneti wa Kamati ya Mambo ya Nje ambao hawakumung'unya maneno baada ya mkutano huo.

"Hapa hakuna bunduki inayofuka moshi - kuna msumeno unaofuka moshi," amesema Seneta Graham akimaanisha mauaji ya Khashoggi yanayodaiwa kutekelezwa kwa kumny'onga kisha kumkata mwanahabari huyo vipande kwa kutumia msumeno.


Seneta huyo amesema hatounga mkono ushiriki wa Saudia katika vita vinavyoendelea nchini Yemen na pia mauzo ya silaha kwa serikali ya Saudia kama bin Salman ataendelea kusalia madarakani.

Seneta Bob Menendez wa chama cha Democrat ameunga mkono msimamo wa Seneta Graham.

Mendez anayetoka jimbo la New Jersey amesema: "Marekani lazima itume salamu za wazi bila kubabaisha kuwa vitendo kama hivyo (mauaji) havikubaliki."

Seneta mwengine kutoka chama cha Republican, akitumia jina maarufu la mwanafalme huyo la MBS amesema: "Sina hata swali moja kichwani mwangu juu ya kuwa MBS aliamuru mauaji hayo (ya Khashoggi)."

Seneta huyo meongeza kuwa : "Laiti MBS angesimamishwa mbele ya mahakama, angehukumiwa ndani ya dakika 30. Anahatia."

CIA 'yamlaumu bin Salman' kwa mauaji ya Khashoggi

Seneta Corker ameonesha wasiwasi wake kuwa rais Donald Trump amepuuzia mauaji hayo kwa kushindwa kumlaani bin Salman.

Bunge la Seneti sasa linapanga kupigia kura mapendekezo ya kusitisha uungaji mkono kijeshi wa Marekani kwa Saudia na washirika wake katika vita inyoendelea Yemen. Tayari wajumbe wa vyama vyote viwili vya Democrat na Republican wameshakubaliana katika hatua ya mwanzo ya pendekezo hilo.

Seneta Chris Murphy, ambaye hakuwepo kwenye mkutano na bi Haspel ameutuhumu utawala wa Trump : "Sio kila kitu kinatakiwa kufanywa kuwa siri," ameandika seneta huyo wa jimbo la Connecticut kupitia chama cha Democrat kupitia mtandao wake wa twitter.

"Kama serikali yetu inajua kuwa viongozi wa Saudia walishiriki mauaji ya mkaazi wa Marekani (Khashoggi) kwa nini umma usiambiwe ukweli?"
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad