Mtu Anasema Yupo Kwenye Foleni Kumbe Analiwa – Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtu Anasema Yupo Kwenye Foleni Kumbe Analiwa – Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wanasiasa wa upinzani na Watanzania kwa ujumla wampongeze pale panapo bidi na sio kila kitu kukosoa na kushindwa kuona mazuri anayoyafanya.



Rais Magufuli amesema hayo leo Desemba 18, 2018 alivyokuwa anahutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa Barabara ya Kimara-Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2.

“Mnapata vigugumizi gani kusema Rais unasimamia vizuri kodi? Mtu anasema hiyo barabara ni kodi zetu, ni kweli, lakini kwani kodi mmeanza kulipa leo? Mbona hazikuwa zinajenga barabara? Si mnipongeze nasimamia kodi vizuri. Na mimi nataka kusifiwa nikiwa hai,” amesema Rais Dkt Magufuli .

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema kuwa ujenzi huo wa barabara utasaidia kupunguza foleni, jambo ambalo limekuwa likivunja ndoa nyingi kwenye jamii.

“Foleni ya barabarani imesababisha hata ndoa nyingine kuvunjika. Mtu anasingizia yupo kwenye foleni, kumbe kuna mtu analiwa, ila sio kuliwa kule mnakokufikiria ninyi.“amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara – Kibaha kwa urefu wa kilometa 19.2, upanuzi wake utakuwa wa njia 6 hadi 8.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad