Reginald Mengi Awamwagia Zawadi Serengeti BoysBaada ya Kutwaa Ubingwa wa Cosafa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Reginald Mengi   Awamwagia Zawadi Serengeti BoysBaada ya Kutwaa Ubingwa wa Cosafa
MLEZI wa Serengeti Boys, Dkt Reginald Mengi mapema leo aliandaa hafla fupi kwa ajili ya kukipongeza kikosi cha Srengeti Boys kilichotwaa ubingwa wa kombe la Cosafa, hivi karibuni nchini Botswana.


Katika hafla hiyo Dkt Mengi aliwapongeza kwa ubingwa huo huku akiitoa zawadi ya fedha kwa wachezaji na benchi zima la ufundi huku akiwaambia kuwa kutwaa kombe hilo ni moja ya safari nzuri ya kuelekea kutwaa ubingwa katika michuano ya Afcon inayotarajiwa kurindima mwakani hapa nchini.


Mlezi wa timu ya Serengeti Boys Dkt, Reginald Mengi, akionyesha kombe hilo baada ya kukabidhiwa na Nahodha wa timu hiyo Moris Abraham kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliyopo ndani ya Hoteli ya Serena Posta jijini Dar es Salaam.

“Hii ni historia kwa timu yetu hii ya vijana kufanya vizuri kwenye Mashindano mawili ikiwemo kombe la Cosafa, hivyo wanastahili pongezi.


Kikosi cha Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys kikiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliongozwa na Waziri Harrison Mwakyembe na Mlezi wa timu hiyo Dkt Reginald Mengi.

“Pia niipongez serikali kwa sapoti kubwa wanayoendelea kuitoa katika timu yangu hii ya vijana, hivyo tutampatia kombe hili mheshimiwa Rais Magufuli kama zawadi ya krismasi, kwani tunajua atafurahia kwakuwa ni mmoja ya viongozi wapenda mafanikio.


Nahodha wa Serengeti Boys Moris Abraham (katikati kushoto na Straika wa timu hiyo, Kelvin John (aliyesimama katikati kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi wa timu hiyo Dkt Reginald Mengi wa kwanza kushoto , pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe wa kwanza kulia.

“Mbali na zawadi hizi nilizotoa hapa naomba niwaambie tu vijana wangu wa Serengeti Boys kuwa zawadi hii ya leo nimelazimika kuipinguza baada ya kushauriwa kuwa umri wenu bado ni mdogo sana hivyo kwakuwa mimi nitaendelea kuwa nanyi, nitatatumia mali zangu zote ili nihakikishe huko badaye maisha yenu yanakuwa mazuri,” alisema Mengi.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad