Serikali yatoa Onyo kwa Wanaotumia Dini Kisiasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaonya baadhi ya watu wanaojipenyeza kupitia mgongo wa taasisi za dini nchini kwa kujifanya wahubiri kumbe ni wachochezi na wanaingiza masuala ya kisiasa kwenye dini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sunsi, Jimbo la Mwibara, mkoani Mara, Lugola ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amesema taasisi za dini zina mchango mkubwa nchini na uwepo wao ni muhimu katika maendeleo ya nchi na serikali inathamini sana mchango wao katika kuimarisha amani na pia kuwaweka watu pamoja.

Amesema kuna baadhi ya dini hizo zinakiuka utaratibu wa usajili na kuvunja sheria za nchi kwa kuacha kuhubiri masuala ya kiroho na kujihusisha na masuala ya kisiasa na uchochezi.

"Kuna baadhi ya makanisa bado hayajasajiliwa kwasababu tunahitaji umakini mkubwa katika kufanya uchunguzi wa kina kabla hatujatoa usajili kwa lengo la kuepusha baadhi ya taasisi za dini zenye mpango mbaya na maendeleo ya nchi", amesema Waziri Lugola.

Ameongeza kuwa,
“Serikali hii haitakuwa tayari kwa mwananchi yeyote kutumia mwamvuli wa dini au kufanya misikiti na makanisa kuwa kichaka kwa kufanya uchochezi nchini na kuhatarisha amani ya nchi tuko makini na hatuwezi kuchezewa na mtu yeyote au taasisiyoyote".
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad