12/01/2018

Sheikh Afungukia Kinachomsibu Rose Muhando


Sheikh Abdulrazack aliyejizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa mlezi wa wasanii mbali mbali ametoa Siri ya nini hasa kinachomsibu Msanii wa nyimbo za Injili Rose Muhando.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Sheikh Abdul Razak amesema kwamba mwanamuziki huyo atakuwa amemkosea Mungu kwa namna yoyote ile, hivyo njia sahihi ya yeye kumaliza matatizo yake ni kupiga goti na kuomba toba.

Akiendelea kuzungumzia hilo Sheikh Abdulrazak amesema kwamba binadamu yeyote ambaye kweli moyoni mwake ana Mungu, hawezi pitia anayopitia Rose Muhando, kwani hakuna uchawi unaoweza kupanda kwenye Mungu, hivyo ni vyema kwa yeye mwenyewe kuamua kumrudia Mungu.

Lazima uelewe kitu kimoja, mtu yeyote ambaye ndani yake kuna nafsi ya ufalme wa Mungu, hawezi kudhuriwa na wachawi, hawezi kudhuriwa na ushirikina, kuna mitihani Mungu atakupa, ni kujaingalia tu wapi alimuacha Mungu, wapi alimkosea Mungu, pale alipomkosea Mungu ndiyo funguo pekee ya yeye kurekebisha hayo yaliyoharinika, yeye mwenyewe Rose Muhando kuna sehemu kamkosea Mungu, hapo ndipo pa kutengeneza, yeye mwenyewe apige goti”.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger