Wajanja Hatulindi Demu, Bali Tunafanya Hivi..!!!!


Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama haupo...Usitumie Nguvu na
Ubabe kumlinda kama hana sababu ya yeye kujilinda mwenyewe.

Mpende na ajue anapendwa ili asiwe na sababu ya kuuchakachua upendo unaompa maana unamtosha kumlinda dhidi ya maupendo feki ya mtaani. Sasa wewe badala ya ku-invest muda wako kumpa Upendo wa kutosha, umejigeuza Alarm, kwamba unaweza kumlinda asiibiwe au asikusaliti...

Unapoteza muda kumfuatilia anaenda wapi, na nani, na kwa nini hajaaga,unamfuatilia nani kamtumia meseji na nani anaongea nae kwa simu mpaka unaenda kuprint statement kwenye mtandao anaotumia... Unapoteza muda wako Kama hujawahi kumiliki hata Shina la Mgomba utawezaje kumiliki mtu???

Mpenzi halindwi kama alarm, watu watai-Snooze na watamuiba kama kawa,Mpe sababu za kujiona anapendwa ili ajilinde mwenyewe. Kumlinda Mpenzi ni sawa na kulinda Bahari,wewe unalinda Coco Beach wenzio wanavua samaki Bagamoyo
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL >BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIALLoading...

Wajanja Hatulindi Demu, Bali Tunafanya Hivi..!!!! Wajanja Hatulindi Demu, Bali Tunafanya Hivi..!!!! Reviewed by Udaku Special on December 08, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.