Aliyezaa na TID Aonyesha Mwanaume Mwingine Anayedai Amezaa Naye

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyezaa na TID Aonyesha Mwanaume Mwingine Anayedai Amezaa Naye
BAADA ya vuta nikuvute kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ na mzazi mwenziye Shekha Mdogo hatimaye mwanamke huyo ameamua kuvunja ukimya na kumwanika baba halisi wa mwanaye.



Akizungumza na Ijumaa Wikienda, kwa njia ya simu akiwa nchini Ujeru­mani, Shekha alisema kuwa anam­shangaa T.I.D anavyokomaa kwamba mtoto ni wa kwake wakati baba halisi ni mwanamuziki wa nchini Kenya, Joseph Makini ‘Prezzo’.



Shekha aliendelea kusema kuwa ameamua kumwanika baba wa mtoto wake kwa sababu amechoshwa na TID kumfuatafuata kwa hiyo kuanzia sasa asahau kabisa kuhusu hilo.

“Nimenyamaza kwa muda mrefu lakini sasa nimeshindwa kabisa kuen­delea kuvumilia ndiyo maana naweka wazi na TID ajue kuwa mtoto siyo wake bali ana baba yake.


“Uzuri ni kwamba Prezzo ambaye ndiye baba wa mwanangu naye ni mwanamuziki hivyo kama TID anataka amuulize mwenyewe atapata jibu kuhusu nani anastahili kuitwa baba wa mtoto,” alisema Shekha.

Aidha alimtaka T.I.D kuendelea na maisha yake na yeye aendelee na maisha yake pamoja na mtoto wake kwa sababu hata baba yake ambaye ni Prezzo anamuhitaji pia hivyo waachane kwa usalama hataki malumbano kwani yeye ndiye alisababisha mpaka mambo hayo yakafikia hapo yalipo sasa.



“Haya mambo yasingefika huku ila TID ndiye aliyesababisha maana anang’ang’ania vitu ambavyo siyo vyake, naomba aniache jamani na mai­sha yangu huyu mtoto ni wa Prezzo nimemaliza,” alisema Shekha.

Ijumaa Wikienda lilimtafuta TID kuhusiana na kauli aliyotoa Shekha kwamba mtoto ni wa Prezzo ambapo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa mtoto huyo ni wake hata aje nani anachojua ndiyo hicho na si kitu kingine chochote.



“Jamani hata aseme nini mtoto ni wa kwangu yeye ataongea mpaka basi lakini ajue mtoto ni wangu hata mtoto atakuwa anajua, huyo Shekha anajidanganya nafsi yake mwenyewe,” alisema T.I.D.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad