Askofu Gwajima Atoa Ushauri Mzito Kwa Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.

Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.

Kwenye ushauri huo Askofu Gwajima ambaye alianza kwa kumsifu Rais Magufuli, amesema kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye 'exposure' kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

“ Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali mbali duniani”, amesema Askofu  Gwajima.

Sambamba na hilo Mchungaji Gwajima ameendelea kueleza kwamba madini tuliyonayo ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.

"Nilipita Mwadui nikashangaa, wakaniuliza tukuletee almasi kwa utani, ndani ya saa moja watu walileta almasi imejaa bakuli haina watu wa kununua, wametoka nazo ndani ya nyumba zao, hizo kama zingelipiwa ushuru nchi yetu ingekuwa mahali pazuri sana”, amesema Gwajima

Hii leo Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo nchini.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad