Ushenzi wa R Kelly Ulidhaminiwa na Wazazi wa Watoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



DOCUSERIES ya Surviving R Kelly inatuma lawama nyingi kwa wazazi. Kutoa uhuru mkubwa kwa watoto na kuwaamini bila kufuatilia.

Aaliyah alipelekwa kwa R Kelly na mjomba wake, Barry Henkerson, prodyuza mwenzake R Kelly. Barry alimfahamu vizuri R Kelly, lakini alimwacha awe jirani na Aaliyah. Matokeo yake R Kelly alimuoa Aaliyah, aliyekuwa na umri wa miaka 15.

Sparkle alikuwa 'back vocalist' wa R Kelly. Walishirikiana katika wimbo "Be Careful" ambao ilikuwa hit matata sana. Hivyo, Sparkle anamjua R Kelly, lakini alimkabidhi mtoto Reshona amlee kimuziki. Mwisho Reshona alinyanyaswa kingono na R Kelly.

Jerhonda stori yake ni jinsi wazazi wake walivyompa uhuru kupita kiasi. Alipowaambia anakwenda kwa rafiki yake, walimkubalia bila kufuatilia, matokeo yake aliangukia kwa R Kelly.

Katika documentary ya BBC yenye jina, "Sex, Girls, STDs: R Kelly Sex Scandal", wameguswa Lisa Van Allen, Faith Rogers, Kitti Jones, Asante McGee na Joycelyn Savage. Hapa nisimulie Joycelyn alivyonasa kwa R Kelly.

Joycelyn anatamani kuwa mwanamuziki. Wazazi wa Joycelyn wapo vizuri kimaisha. Jumba la kifahari Atlanta, wanaendesha magari ya bei mbaya. Hawana njaa. Walipoona mtoto wao kipaji chake ni muziki, waliamua kumtafuta R Kelly ili amsaidie mtoto wao kumuingiza kwenye lebo.

Baba wa Joycelyn, Tim Savage na mama yake, Jonjelyn Savage, walipata namba ya R Kelly ambaye alikubali kumpokea binti yao. Faith Rogers alipofanikiwa kuchomoka kwenye jengo la R Kelly, aliwatafuta wazazi wa Joycelyn na kuwaeleza kinachoendelea mjengoni kuwa mtoto wao anashiriki mapenzi ya kikundi na R Kelly.

Faith aliwaambia kuwa R Kelly ana maambukizi ya magonjwa ya ngono (STDs). Na alithibitisha hivyo kwa kuwa baada ya kutoroka, alipima na kukutwa na STDs.

Baada ya hapo, wazazi wa Joycelyn walitumia jitihada nyingi kumpata binti yao bila mafanikio. FBI waliingilia kati lakini Joycelyn hataki kurudi kwa wazazi wake.

Tunarudi kulekule, wazazi wa Joycelyn walijua kila stori kuhusu R Kelly, lakini wakampeleka. Mpaka leo wanaendelea na mapambano ya kumpata bila mafanikio. Mtoto kaganda kwa R Kellyelly. Ni makosa ya wazazi wenyewe.


Ndimi Luqman MALOTO
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad