Serikali yafuta Umiliki wa Mashamba Sita ya Mo Dewji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula leo Jumatatu ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa ekari 12, 915. 126 ya kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL) yaliyopo Korogwe jijini Tanga.

Taarifa ilitolewa kwa umma na kitengo cha mawasiliano cha wizara hiyo imesema uamuzi wa kufuta mashamba hayo umefikiwa baada ya mapendekezo yaliyotolewa na halmashauri ya wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.

Imesema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Rais John Magufuli na wizara kwa nia ya kufutwa mashamba hayo ya MeTL  ambayo ofisa mtendaji mkuu wake ni bilionea namba moja kijana barani Afrika, Mohammed Dewji ‘Mo.’

Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliyopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo, Mabula amesema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises, Mazinde wilayani Korogwe.

Amesema uamuzi huo unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za Serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji.

Amesema mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohammed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji katika halmashauri husika kuhusu kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa Rais na kuridhiwa.

Mabula amesema uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohammed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji. 

Naibu waziri huyo amesema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri.

Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.

Mabula amempongeza mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella kwa kufanya kazi nzuri ya kufuatilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga.

Kwa upande wake, Shigella amewataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo halmashauri ya wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo.

Amesema ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad