Hii Hapa Hali ya Mzee Sumaye Baada ya Kuugua Ghafla Akiwa Mkoani Tanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Frederick Sumaye anaendelea vizuri na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) alikohamishiwa Jana Usiku baada ya kupokelewa Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Mkoa wa Tanga jioni ya jana.

Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Mhe. Freeman Mbowe ambaye bado yuko mahabusu Gereza la Segerea pamoja na Mbunge Esther Matiko, amemtumia salaam za pole na kumtakia uponaji wa haraka Mzee Sumaye ili arejee katika majukumu yake.

Aidha, Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Patrick Ole Sosopi pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho ngazi na maeneo mbalimbali ya nchi, wamefika hospitalini hapo kumjulia hali na kumpatia pole Mzee Sumaye ambaye pia Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad