2/11/2019

Nisha Awatolea Povu Wanaoisakama Shepu Yake


Msanii wa filamu na muziki wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ameibuka na kuwajia juu watu ambao wamekuwa wakimsema kuwa shepu yake ni feki.

Sakata hilo lilijitokeza siku chache zilizopita baada ya Nisha kuweka picha katika ukurasa wake wa kijamii iliyomuonyesha akiwa na shepu na umbo namba nane ambayo hakuwa nayo kwenye picha zake nyingine.Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha alisema watu wamekuwa wakichonga sana hivyo amewaachia nafasi waendelee kwani hawamuongezei wala kumpunguzia chochote.

Hao mashabiki nimewaacha tu wazidi kushambulia kwa sababu bando ni lao, simu ni zao, mimi sijali chochote maana kujibishana na watu ni kupoteza muda kwenye vitu ambavyo siyo muhimu wala havina faida kwangu”.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger