2/18/2019

VIDEO: Maajabu..Mfanyakazi wa Benki Aishi na Lundo la Taka Chumbani Kwake

Mtu mmoja mkazi wa Buguruni kwa madenge aliyefahamika kwa jina la Salum amegundulika kuwa anaishi na lundo la takataka chumbani kwake kwa muda mrefu sasa

Bw. Salum ambaye inasemekana kuwa ni mfanyakazi mstaafu wa Bank, amegundulika kuwa anaishi na lundo hilo la takataka chumbani kwake baada ya kuonekana kuna dalili za moto kuwaka kutokea chumbani humo huku yeye akiwa safarini mkoni Morogoro

Baadhi ya wakazi pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa huo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku wakiwa hawajui sababu ya mpangaji huyo kuweza kuishi na lundo hilo la takataka kipindi chote hicho. Wakiendelea mbele zaidi wakazi hao wanasema kuwa jirani yao huyo hakuwa anaonyesha dalili yoyote kwamba anaishi na uchafu huo chumbani kwake.

Inavyosemakana moja ya tabia aliyokuwa nayo Bw. Salum ni kupenda kugawa pesa za shilingi elfu tano ( 5,000 ) kwa watoto wa mtaa huo bila kujali wingi wa watoto hao huku kila mmoja akimpa kiasi hicho cha pesa hata kama watakuwa watoto ishirini

Wewe unalizungumziaje jambo hilo? tuachie comment yako hapo chini na usisahau kusubscribe na kubonyeza alama ya kengere ili uwe wa kwanza kupata taarifa zote

Tazama VIDEO:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger