Jerry Muro Afunguka Kuhusu Kumng'oa Mbowe Jimbo la Hai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jerry Muro Afunguka Kuhusu Kumng'oa Mbowe Jimbo la Hai
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amezungumzia mpango wake wa kuwania Ubunge katika jimbo la Hai kweye Uchaguzi Mkuu 2020, ambalo kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe ambapo amesema suala hilo linahitaji neema za Mungu.


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Break Fast cha East Africa Radio, Jerry Muro amesema ni kweli kumekuwa na maneno ya watu wengi wanaodai kuwa anaonekana mara kwa mara akifanya harambee kwenye jimbo la Hai.

Swali

Mtangazaji Charles William, "ukiwa jijini Dar es salaam ulionekana ukijitambulisha kama mkazi wa Ubungo Maziwa na mara kwa mara ulionekana ukimkosoa Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, na sasa unaonekaa umelenga kuingia jimbo la Hai ni kweli unalitaka jimbo lile"?

Majibu

Jerry Muro, "hakuna binadamu anayeishi bila matamanio, mimi siwezi kusema matamanio yangu ni nini lakini Mungu akisema uwe Mbunge utakuwa lakini akisema usiwe Mbunge hata ufanye harambee 500 hutakuwa Mbunge, niwaambie watanzania masuala ya Ubunge yanahitaji kumtazama Mungu".

"Wanaokwambia Jerry Muro anataka Ubunge ujue wanamatamanio mimi niwe Mbunge wao, kwa hiyo kama wewe unajua mwambie Mbowe ikiwaka mulika, ikizimika papasa".ameongeza Jerry Muro

Jerry Muro alipata umaarufu mkubwa alipokuwa Msemaji wa Klabu ya Soka ya Yanga kabla ya kuachana nayo na kuteuliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad