Mboso Afanya Shopping ya Nguvu Awashukuru Mashabiki Wake kwa Kupata Tuzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mboso Afanya Shopping ya Nguvu Awashukuru Mashabiki Wake kwa Kupata Tuzo
Mwanamuziki wa kizazi kipy, Yusuf Kirungi maarufu kwa jina la Mboso, amewashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kutwaa tuzo ya video bora ya wimbo wake wa hodari iliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda.



Mboso amesema tuzo hiyo imempa nguvu ya kufanya vizuri zaidi baada ya kimya cha muda mrefu na kwamba siku chache zijazo ataachia kitu kipya ambacho kitakuwa cha mshindo mkuu katika anga ya muziki wa Tanzania na kuwapa majibu wanaodhani kwamba ameanza kupotea katika anga ya muziki.



Msanii huyo ameeleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wetu, alipokutana naye katika duka maarufu la Pugu Mall, alikokwenda kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali yakiwemo mavazi akiwa ameambatana na baadhi ya wapambe wake, huku akiwa miongoni mwa wanufaika wa punguzo la asilimia 20 ya bidhaa kwenye duka hilo.



Naye Meneja Uhusiano wa Pugu Mall, Matina Nkurlu akizungumzia hatua ya mwanamuziki huyo kutembelea duka hilo na kufanya manunuzi alisema anashukuru sana msanii huyo kufika katika duka hilo na kufanya manunuzi ya nguo na vitu mbalimbali na kujipatia punguzo la  asilimia 20 huku akiwataka mastaa wengine kufika kwenye duka hilo ili wajipatie ofa hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad