Simba yaendeleza ubabe, yairarua Ruvu Shooting 2 – 0

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalifungwa na Paul Bukaba dakika ya 52 pamoja na Meddie Kagere dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kufikisha alama 54 nafasi ya tatu katika michezo 21 ya Ligi Kuu ikishinda michezo 17, sare michezo 3 na kupoteza mchezo 1, Azam FC ikiwa nafasi ya pili kwa alama 59 katika michezo 28, ikishinda michezo 17, sare michezo 8 na kupoteza michezo 3, huku Yanga SC ikiendelea kusalia kileleni kwa alama 67 katika michezo 28 ikishinda michezo 21, sare michezo 4 na kupoteza michezo 3.

Simba waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu za kutoka kufuzu kucheza robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya AS Vita.

Huwenda wangeweza kupoteza mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting au kutoka sare kutokana na uchovu dhidi ya game yao ya mwisho ya makundi ya CAF Champions League, lakini Simba SC wameendeleza vichapo kwa kuifunga Ruvu Shooting magoli 2-0.

Wakati Simba SC wanaendelea kuwa nafasi ya 3 wakiwa na point 54, bado wana viporo 7 vya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad