Atletico Madrid 'Yamfukuza' Diego Costa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KLABU ya Atletico Madrid ipo tayari kumuuza straika wake, Diego Costa kutokana na utovu wa nidhamu lakini kocha wake, Diego Simeone anataka abaki.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Atletico wamechoshwa na tabia zake ambazo zimekuwa zikiigharimu timu huku uwezo wake uwanjani ukiwa hauridhishi pia.

Msimu wa Costa kwa sasa umeshamalizika kwa kuwa amefungiwa kutocheza mechi nane kutokana na kumtukana mwamuzi katika mchezo dhidi ya Barcelona, mapema mwezi huu. Upande wa Simeone ameshikilia msimamo wake kuwa bado anamuhitaji mchezaji huyo licha ya kuwa amekuwa na matatizo kadhaa.

Costa alimtolea lugha kali mwamuzi, Gil Manzano huku akimshika na kumtikisa kwenye mikono, baada ya kupewa kadi nyekundu na timu yake ilifungwa mabao 2-0. Simeone hakumtetea Costa kwa kile alichokifanya lakini bado anaona ni mchezaji sahihi kuendelea kubaki kikosini hapo.

Hii ni mara ya pili Costa anaitumikia timu hiyo, awali aliondoka kwenda Chelsea lakini akarejea klabuni hapo kwa ada ya pauni 53m mwaka 2017. Amefunga mabao matano katika mechi 21 za michuano yote alizocheza
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad